Monday, July 30, 2018

PRE SEASON KURINDIMA JIJINI MWANZA UWANJA WA NYAMAGANA.

BUDA MTANZANIA, MWANZA

Mashiandano ya Maandalizi ya Msimu kwa Timu za Kanda ya Ziwa yaliyopewa jina la Preseason Tournament 2018,yanatarajiwa kutimua Vumbi August 4 Mwaka huu katika Dimba kongwe la Nyamgana jijini Mwanza.

Akizungumza na Website ya Famara News Mjumbe wa kamati ya mashindano hayo Cathbert Japhet amesema maahindanaoa hayo yako chini ya Kàmpuni ya Clevalend Resources kwa kushirikiana na Chama cha soka Jijini Mwanza,ikiwa ni lengo La kuziandaa timu zitakazoshiriki ligi kuu Tanzania Bara msimu 2018-2019 huku zikishirikisha jumla ya Timu nne.

"Kupitia kwa Mkurugenzi wa Cleveland Resources ndugu Kabole Kahungwa tumeamua kuyaleta mashindano haya katika Jiji la Mwanza baada ya kufanyika katika Mkoa Wa Shinyanga katika misimu kadhaa iloyopita"amesema Cathbert

Kwa upande wake Mwakilishi Wa chama cha soka jijini Mwanza MZFA Mwalimu Erastus Mayala amewapongeza waandaaji Wa michuano hiyo huku akivitaka Vilabu kujitokeza kwa Wingi katika mashindano haya.

Mashindano haya yatafanyika kwa Mara ya kwanza katika Jiji la Mwanza na kuzishirikisha Timu za Mbao fc ya Mwanza,Mwadui fc ya Shinyanga,Kagera Sugar ya Kagera na Gipco ya Geita ambao ni mabingwa wa Mkoa Wa Geita,huku Mshindi wa mashindano hayo atakayepatikana kwa njia ya points atakabidhiwa kikombe na mshindi wa pili akiambulia medali za heshima.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: