Tuesday, July 24, 2018

POGBA KUMFUATA CRISTIANO RONALDO JUVENTUS

Nyota wa Manchester United, Paul Pogba ameiyambia klabu yake kuwa anahitaji kurejea katika timu yake ya zamani ya Juventus kwenda kucheza pamoja na Cristiano Ronaldo ambaye amejiunga na klabu hiyo siku chache zilizopita.

Pogba amemueleza wakala wake kuwa anahitaji kurejea ndani ya Juve kwenda kucheza na Ronaldo, japo kuwa nyota huyo anahusishwa kutakiwa na klabu ya Barcelona.

Miaka miwili iliyopita klabu ya United ilitoa kiasi cha euro milioni 114 kukamilisha usajili wa Mfaransa huyo ambaye alikuwa akiichezea klabu hiyo ya Juventus.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: