Wednesday, July 25, 2018

POGBA ANAWAJIBU WAKUONESHA KIWANGO BORA - MOURINHO

Meneja wa Manchester United ambaye yupo na kikosi chake nchini Marekani kwa ajili ya maandali ya msimu mpya wa 2018/19 amefunguka nakusema kuwa kiungo wake Paul Pogba anawajibu wakuonesha kiwango kikubwa kama alivyoweza kuonesha kwenye Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya Taifa ya Ufaransa.

"Suala sio timu kubadilika ili kumfanya Pogba atoe kitu bora ni wajibu wake yeye kutoa kile bora alichonacho kwa ajili ya timu kama ambavyo amefanya huko kwingine" Amesema Mourinho.

Lakini Mreno huyo amesema kuwa hajashangazwa na kiwango cha Poga katika fainali za kombe la Dunia kutokana na mashindano hayo kuwa ya mwezi mmoja na hivyo mchezaji anakuwa anawaza mechi tu, na anakuwa kambini muda wote na hanakuwa hana nafasi ya kujua mengi ya nje ya uwanja.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: