Monday, July 16, 2018

PICHA: SHEREHE ZA KOMBE LA DUNIA UFARANSA ZAUA NA MAELFU YA WATU KUJERUHIWA

Wakati furaha ikiendelea kwa Taifa la Ufaransa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia nchini Urusi hapo jana usiku, sherehe za ubingwa huo zimeleta maafa nchini Ufaransa.

Kwa mujibu gazeti la Daily Mail limeripoti kuwa mpaka asubuhi ya leo watu wawili wmeishafariki dunia kwenye mlundikano na maandamano makubwa yaliyofanyika mjini Paris katika viwanja vya Champs Elysees.

Taarifa zinaeleza chanzo cha vurugu na mkanyagano ni Polisi wa mjini Paris, Nancy na Lyon waliokuwa wanatumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya washawasha kuwatawanya watu wliokuwa wanashangilia kwa maandamano barabarani.

Taarifa zinaeleza kuwa zaidi ya watu milioni moja walikusanyika katika viunga vya Jiji la Paris kuuzuguka mnara wa Eiffel.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: