Friday, July 27, 2018

"NITAWATOA MATUMBO KABLA TUMBO LANGU HALIJATUMBULIWA" - LUGOLA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amevionya vyama vya siasa kwa kusema hayuko tayari kutumbuliwa kwa sababu ya kushuhudia mtu yeyote akitoa lugha za kichochezi kwa kisingizio cha kumnadi mombea jukwaani. 

Lugola ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, amesema kuwa mgombea atakayetoa matamshi ya uchohezi atakamatwa na huenda akakosa haki ya kuendelea na uchaguzi.

"Siko tayari kutumbuliwa ila niko tayari kuwatoa matumbo wote watakaokuwa wanajishughulisha na uchochezi kabla tumbo langu halijatumbuliwa na Mheshimiwa Rais" Amesema Kangi Lugola.

Kauli hiyo ya kuvionya vyama vya siasa imekuja wakati vyama hivyo vikiwa kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa madiwani na ubunge utakao fanyika Agosti 12.

Waziri Lugora ameongeza kwa kusema kuwa hayuko tayari kumuangusha Rais kwakuwa katika kiapo chake, wakati anaapishwa aliahidi kuwalinda watanzania, kudumisha amani na usalama wa nchi.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: