Monday, July 16, 2018

MTAZAMO WANGU- MSHINDI WA BALLON D' OR 2018.Na Mandala J.

Huyu hapa kwangu Mimi ndie mshindi sahihi wa zawadi ya mchezaji bora wa Dunia. Ndie mchezaji mwenye sifa kimpira japo si kibiashara.

Luka Modric amechukua European Champions Leaque Mara tatu mfululizo akiwa na Zinedine Zidane na Real Madrid ya akina Christiano Ronaldo. Ni Luka Modric ndie anaeifanya Real Madrid iwe kama ilivyo na iweze kushinda katika michezo migumu na ukitaja wachezaji watatu walioisaidia Real Madrid kuwa mabingwa Mara tatu mfululizo wa UCL hutakosa kumtaja na yeye.

Mwaka 1998 Real Madrid walishinda UCL na Trance walishinda World Cup mshindi aliibuka Zinedine Zidane japo mfungaji bora alikuwa Davor Suker , Zinedine Zidane alikuwa kiungo wa Juventus  , mwaka 2002 mabingwa wa UCL walikuwa Real Madrid na goli la ajabu la Zinedine Zidane baada ya kuwafunga Bayern Leverkusen ya akina Lucio , Brazil walibeba kombe la Dunia pale Korea Kusini na Japan na aliekuwa mchezaji wa Inter Milan Ronaldo Luis Nazario De Lima ndie alieibuka mfungaji bora wa kombe la dunia kwa magoli 8 lakini waliobeba Kombe la mabingwa Ulaya walikuwa Real Madrid.  
Fabio Canavarro aliibuka mshindi mwaka 2006 baada ya kushinda World Cup akiwa na Italia na mchezaji wa  Real Madrid lakini UCL ilienda kwa Barcelona baada ya kuwafunga Arsenal pale Stade De France.
Ukiangalia pia mafanikio makubwa katika kombe la dunia ilikuwa kama alama sahihi ya sifa  kubeba Ballon D' Or  Kama hawa  walishinda  kwa sifa hizi?
Kombe la dunia mwaka 2010 ndipo tulianza kuona kama sifa hii kuondoka na hasa baada ya Andreas Iniesta kuwa katika kiwango bora kutopewa ushindi na ushindi kwenda kwa Lionel Messi wa Argentina ambae timu yake haikufika wala fainali ya mashindano haya hata hivyo msimu wa mwaka 2010 kombe la mabingwa Ulaya lilienda kwa Internationale Milan ya Jose Mourinyo mwaka 2011 lilienda kwa Barcelona ya Lionel Messi na Kombe la Dunia mwaka 2014 lilienda Ujerumani na Portugal haikuvuka hata makundi ila misimu inaweza kukuchanganya ila ukweli ni kwamba Ballon D or ikikuja na sura ya kibiashara kwa makampuni yanayowadhamini Lionel Messi na Christiano Ronaldo katika vifaa vya mpira.
 Nashani kuna haja ya kurudi katika sifa za kimpira zile zilizowapa sifa akina Ronaldo de Lima, Zinedine Zidane na Fabio Canavarro na kuachana na utamaduni huu wa akina Lionel Messi na Christiano Ronaldo na kumpa sifa hizo  Luka Modric kushinda hata kama hatabeba kombe la dunia, kufika fainali ya kombe la dunia we mshindi hivyo basi nae anastahili . Pamoja na Raphael Varane atakuwa na makombe mawili kama France watakuwa mabingwa na ukweli ni kwamba kombe la dunia ni kombe kubwa kuliko UCL lakini mchango wa Raphael Varane katika timu ya Real Madrid na France ni mdogo kuliko huduma anayoitoa Luka Modric pale Real Madrid na Croatia.

Unaweza ukasema kuwa mbona Andreas Iniesta au Xavi Hernandez walikosa kuwa washindi lakini miaka waliokuwa katika kiwango ilikuwa ni miaka ambayo uwezo na mafanikio ya Lionel Messi au Christiano Ronaldo yalikuwa juu sana na sifa za kibiashara zilichukua nafasi kubwa na kufanya wao kukosa nafasi kwa image au sura ya kibiashara, ni sawa Christiano Ronaldo amepata UCL na kuwa mfungaji bora yaani

Magoli 17 UCL
Magoli 22+ La Liga 
Magoli 4 Kombe La Dunia 
Mshindi wa UCl 

Ukiona mafanikio makubwa ameyapata kombe la mabingwa  Ulaya ambalo lilichangiwa sana na uwezo wa Luka Modric aliekuwa mhimili mkubwa katika timu ya Real Madrid na ndio maana ukitaja wachezaji watatu utaacha kumtaja Christiano Ronaldo, Luka Modric wa mwisho unamjua ndio waliochangia sana Real Madrid kuwa mabingwa wa UCL.

Lionel Messi 
Mshindi la Liga
Mfungaji bora Ulaya
Supper Coppa
Mchezaji mzuri mtengenezaji

Hizi ni sifa ambazo hazina ukubwa dhidi ya kile alichofanya Luka Modric akiwa pale Real Madrid na Croatia.

Kama kweli watoaji wa zawadi hii walijifunza kwa kile walichomfanyia Phillip Ram pamoja na kuwa bingwa wa Dunia , Bundesliga na UCL bado hakuwa mshindi.

Ni sawa Eden Hazard amekuwa mchezaji bora wa mashindano kwa upande wangu na mchezaji mzuri katika michezo mitatu si hapa na anastahili kuwa mchezaji bora wa mashindano lakini pia nikumbushe kwa Sera na siasa za Real Madrid usishangae kwa lolote .

CROATIA wanastahili kuwa bingwa wa kombe la Dunia 2018.

Luka Modric anastahili kuwa mchezaji bora wa Dunia.

Kila kheri Croatia na Luka Modric.

Ahsanteni.

+255659797279
+255620639779.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: