Tuesday, July 24, 2018

MOTO MKUBWA WAZUKA UGIRIKI WAUNGUZA MSITU NA KUUA WATU 20

Moto mkubwa uliozuka na kuunguza msitu nchini Ugiriki umeua watu 20 huku mamlaka ya nchini humo zikisema kuwa zinahitaji msaada wa kimataifa ili kukabiliana na moto huo.

Vikosi vya zima moto mpaka sasa vinaendelea na jitihada za kuuzima moto huo huku watu wakiwa wameyakimbia makazi yao katika maeneo yakaribu na mji mkuu wa taifa hilo Athens.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alex Tsipras amesema watafanya lolote linalowezekana kibanadamu kuhakikisha wanaokoa maisha ya watu.

Idadi ya watu 104 wamejeruhiwa kati yao 11 wakiwa na hali mbaya, laikini watoto 16 wamejeruhiwa.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: