Monday, July 23, 2018

MO DEWJI AIOMBEA KLABU YA YANGA

Mohammed Dewji ambaye ni mfanya biashara mkubwa na maarufu Tanzania ambaye wengi wanamfahamu kwa jina la MO Dewji ameguswa na hali ambayo sio ya nzuri inayoendelea katika klabu ya Yanga.

MO Dewji amefunguka na kusema kuwa anaiombea klabu ya Yanga ili iweze kupita katika kipindi hikin kigu ili iweze kuimarika na kupata timu ya Taifa Stars iliyoimarika.

"Tunahitaji Yanga imara ambayo inaweza kushindana na Simba, tunahitaji Yanga imara kwa ajili ya timu ya Taifa Stars. Ninawaombea Yanga waweze kupita katika kipindi hiki kigumu kwao, wanapaswa watulie na waungane upya"Ameandika mtaalamu MO Dewji katika ukurasa wake wa Twitter.

Kumbuka mpaka sasa MO Dewji ni mmoja wa watu wenye hisa nyingi katika klabu ya Simba SC.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: