Friday, July 20, 2018

MHESHIMIWA STANSLAUS MABULA_ JIMBO LA NYAMAGANA MKOANI MWANZA, KUNG'ARA KWA MAENDELEO.LUCY NKYA, MWANZA

Mbunge Wa Nyamagana Stansiaus Mabula amewataka Wananchi Wa Jimbo la Nyamagana wawe wapole katika Kukamilishiwa Miradi ya Maendeleo ambayo aliwaahidi Kipindi anagombea Kuwa Mbunge.

Akizungumza Na Waandishi Wa Habari ,amesema Kuwa amezitatua Baadhi Ya Changamoto za Wananchi Kwa Miaka Miwili Tangu Achaguliwe na akizitaja kuwa  ni  Pamoja Na Kujenga Madarasa kwa Baadhi Ya Shule Katika Jimbo hilo, kujenga Matundu Miambili Na Themanini Na Sasa Ujenzi Wa Barabara Unaoendelea ukiwa na bajeti ya Shilingi Bilioni Tisa.

Mabula Ameeleza Kuwa Lengo Lake Kubwa Ni kuhakikisha Kuwa Wananchi wanajengewa Zahanati Na Vituo Vya Afya Katika Sehemu Ambazo Hazijawa na Hudumu Hiyo, na amesema kuwa tayari Wamejenga Zahanati Mbili kwa ajili ya  Huduma Ya Afya .

Hata Hivyo Mheshimiwa Mabula amewashukuru Waandishi Wa Habari Kwani Wamekuwa Wakifanya naye Kazi Bega Kwa Bega, Kusaidia Kuwafikishia  Habari  Wananchi Wa Sehemu Mbali Mbali Katika Jimbo La Nyamagana. 


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: