Friday, July 27, 2018

MBWANA SAMATTA KUTUWA LIGI YA HISPANIA

Klabu ya Levante inayoshiriki ligi kuu ya nchini Hispania ipo kwenye harakati za kuhakikisha inafanikiwa kupata saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ili waweze kuimarisha kikosi chao kwa maandalizi ya Ligi.

Klabu hiyo imetenga imemtengea kitita cha euro 4 milioni ili kumsajili Samatta lakini klabu yake ya KRC Genk ya Ubeligiji imekataa ofa hiyo na kusema inahitaji kiasi cha euro 8 milioni ili waweze kumuachia nyota huyo.

Hata hivyo wakala wa Samatta amethibitisha kuwepo kwa mazungumzo kwa klabu hizo, huku klabu ya CSKA Moscow imetajwa kuhitaji huduma ya Mbwana Samatta.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: