Tuesday, July 31, 2018

MBUNGE WA CHADEMA JULIUS KALANGA AJIUZULU NA KUHAMIA CCM

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Monduli kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Julius Kalanga amejiuzulu nafasi yake na kujiunga na Chama cha CCM kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na kudai kuwa ameondoka CHADEMA kwasababu ya siasa za chuki na uhasama.

"Siasa za uhasama, malumbano na chuki zimeniondoa CHADEMA, nimeamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa maslahi ya taifa. Kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili, lazima utaonekana msaliti tu, watu wa Mondoli naombeni mnielewe, nitakuja kuzungumza nanyi" Amesema Julius Kalanga.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: