Tuesday, July 31, 2018

MBOWE AFUNGUKA BAADA YA WABUNGE KUKIHAMA CHAMA HICHO

Wakati lile joto la kisiasa likiwa limepamba moto kwa wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kukihama chama chao na kukimbilia CCM, Mwenyekiti Freeman Mbowe amesema hatishiki juu ya hilo bali anaona wanazidi kukiimarisha na kuwa na nguvu zaidi.

Kauli hiyo ya Mbowe imekuja baada ya matukio ya Wabunge wa CHADEMA pamoja na madiwani kujivua nafasi zao katika nyakati tofauti tofauti na kujiunga na chama tawala (CCM) kwa lengo la kumuunga mkono Rais Magufuli katika utendaji wake wa kazi.

"Wale wanaokimbilia vyama vingine wanakiimarisha zaidi chama chetu kwa sababu kina tupa fursa ya kubaki na viongozi na wanachama wenye uchungu na nia ya dhati ya kukijenga chama chao. Wanaofika bei kwa ahadi ya fedha au vyeo waondoke mapema na nina wahakikishia CHADEMA itaendelea kuwa taasisi imara zaidi kuliko ilivyo sasa" Amesema Mbowe.

Ndani ya siku tatu Wabunge wawili wameachia nafasi zao kutoka CHADEMA wakielekea CCM ambapo jana Julai 30,2018 aliyekuwa Mbunge wa Monduli Julius Kalanga alitangaza kurudi CCM, na Julai 28,2018 aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara alitangaza kuachana na chama hicho.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: