Friday, July 6, 2018

Majukumu yawafunga goli moja kwa bila Msoto, Kombe la Meya ,wenyewe wasema Mwamuzi kawaonea.


TIMU ya Majukumu jana iliikuba mshindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Msoto zote za Vijibweni,halmashauri ya Kigamboni katika mashindano ya kombe la Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.
Mchezo huo ukiwa ni mwendelezo wa mtoano katika hatua ya makundi, kabla ya kuingia robofainali ulipigwa katika uwanja wa Mzimu uliopo Vijibweni hapo jana.
Goli la timu ya Majukumu lilifungwa dakika ya 22 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wao Shabani Kandecha na hivyo kuamsha mashabiki wa timu hiyo waliokuwa wakisubiri kwa bashasha ushindi huo.
Goli hilo lilidumu hadi dakika 90 za mchezo licha ya wapinzani wao kupata penati dakika ya 30 kipindi cha pili lakini hawakuweza kupata goli la kusawazisha.
Hata hivyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, wachezaji wa timu ya Msoto walimlalamikia mwamuzi wa mchezo huo kwakile walichodai kuwa hakuchezesha sawa mchezo huo.
Nahodha wa timu ya Msoto,Mchata Hasani,alisema kuwa mwamuzi wa mchezo huo hakuwa sawa alipochezesha mchezo huo kwani walishinda magoli lakini aliyakataa.
Alidai kuwa walishafungwa mechi mbili kwenye uwanja huo ,lakini hawakuwahi kulalamika dhidi ya matokeo na kwamba mchezo ulikuwa mzuri lakini mwamuzi aliharibu kwakuwa tayari alikuwa na matokeo yake.
“Kiukweli leo refa katuonea,tumepiga mpira umefika golini, kipa kageuka mwamuzi kasema sio goli,tumekosa penati sawa tunakubali lakini katunyima magoli ambayo tulifunga” alisema Mchata.
Mathayo Msongolo ambaye ni mchezaji wa timu hiyo alidai kuwa ,Msoto ndio timu pekee inayo ongoza kwa nidhamu katika kata ya vijibweni na kwamba watafikisha malalmiko yako kwa wahusika wa mashindano hayo kutokana na mwamuzi kupendelea timu moja.
Hata hivyo mwamuzi wa mchezo huo hakuwa tayari kuzungumzia malalamiko yaliyotolewa na timu ya Msoto,huku mwalimu wa timu hiyo pia alisema hawezi kusungumza kwakuwa kashazungumza sana.
Ligi hiyo inaendelea tena leo,ikiwa ni zamu ya kundi D ambapo timu ya Monako ya Vijibweni itamenyana na timu ya Dar United kutoka kwa Azizi Ally halmashauri ya Temeke.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: