Tuesday, July 24, 2018

MAJINA 10 YA WACHEZAJI WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA YATANGAZWA, NEYMAR, POGBA WAANGUKIA PUA

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza majina 10 ya wachezaji wa kiume watakaowania tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa dunia wa mwaka 2017/18.

Lakini katika orodha ya majina iliyotajwa imewashangaza mashabiki wengi baada ya kukosekana kwa majina ya wachezaji nyota waliotazamiwa na wengi, Neymar na Pogba wote wametemwa katika orodha iliyotolewa.

Orodha ya majina hayo ni Cristiano Ronaldo (Juventus), Lionel Messi (Barcelona), Kelvin De Bruyne (Man City), Antoine Griezman (Atletico Madrid), Eden Hazard (Chelsea), Harry Kane (Spurs), Kylian Mbappe (PSG), Luka Modric (Real Madrid), Mohamed Salah (Liverpool) pamoja na Raphael Varane (Real Madrid).

Kitu usichokijua nikuwa majina haya yameanza kuchujwa tokea Julai 3, 2017 hadi Julai 15, 2018 na tuzo zitatolewa mwezi Septemba 24, 2018 Jijini London Uingereza.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: