Tuesday, July 31, 2018

Likizo ya uzazi kwa Wanaume si yakwenda kunywa pombe - Waziri Ummy

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wanaume kutoitumia likizo ya siku tano ya uazazi kwenda kunywa pombe.

Waziri Ummy amesema ataifuta likizo hiyo kwa wanaume endapo atajiridhisha haina manufaa na inatumika ndivyo isivyo.

Akizungumza kuhusu wiki ya Unyonyeshaji itakayoanza siku ya kesho hadi ifikapo Agosti 8 mwaka huu, Waziri Ummy amesema likizo hiyo ni kwa ajili ya kumsaidia mama anapokuwa amejifungua na si vinginevyo.

"Likizo ya uzazi kwa wanaume si yakwenda kunywa pombe, lakini iwapo wanaume wanachua likizo hiyo na nyumbani hawaonekani, nitafanya utafiti kuangalia iwapo ina manufaa kama hakuna tutaifuta" Amesema Waziri Ummy.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: