Monday, July 23, 2018

KIONGOZI MWINGINE MKUBWA YANGA AJIUZULU

Wakati sintofahamu ikiendelea kwenye klabu ya Yanga na kukiwa na wimbi la viongozi wao kujiuzulu, pigo lingine limeikumba klabu hiyo baada ya aliyekuwa kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga kutangaza kujiuzulu nafasi yake.

Sanga amewasilisha barua kwenye uongozi wa timu hiyo akiomba kujiuzulu nafasi yake ya Kaimu Mwenyeketi aliyoitumikia kuanzia mwaka 2017 alipojiuzulu mwenyekiti Yusuf Manji, lakini pia amejiuzulu nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.

Clement Sanga ametoa sababu kubwa iliyopelekea kuchukua uamzi huo ni kutokana na video iliyosambaa mitandaoni hivi karibuni ikionesha mashabiki wa timu hiyo wakiamasishana kwenda na mapanga kumfanyia fujo nyumbani kwake.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: