Monday, July 16, 2018

KEANE AFUNGUKA SABABU ZA ENGLAND KUFUNGWA NA UBELGIJI KOMBE LA DUNIA

Nahodha wa zamani wa klabu ya Manchester United Roy Keane ametaja sababu zilizoipelekea timu ya Taifa ya England kufungwa na Ubelgiji katika mchezo wakusaka mshindi watatu wa Kombe la Dunia.

Keane amesema kuwa kilichoiponza England ni uzembe wa mabeki ambao ni Danny Rose na Phil Jones aliodai kuwa walicheza chini ya kiwango na kupelekea timu hiyo kupoteza mchezo huo wa kutafuta mshindi wa tatu.

Keane alitoa kauli hiyo wakati akichambua mchezo huo ambao ulikuwa nimchezo wapili kwa timu hizo kukutana kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia, ambapo mchezo wakwanza ulikuwa ni wahatua ya makundi na England alikutana na kipigo cha bao 1-0.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: