Monday, July 9, 2018

JUSTIN BIEBER AMVISHA PETE YA UCHUMBA MCHUMBA WAKE

Msanii maarufu wa muziki Duniani Justin Bieber amemvisha pete ya uchumba Mchumba wake anayefahamika kwa jina la Hailey Baldwin.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa wawili hao walivishana pete hiyo nchini Bahamas na kwenye tukio hilo hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kurekodi kwa njia ya simu.

Pia Baba yake na mrembo Baldwin kupitia ukurasa wake alithibitisha taarifa hizo lakini baada ya muda mfupi alifuta Tweet.

Mama yake Justin Bieber naye aliandika kitu kwenye ukurasa wake wa Twitter kuashiria kuwa kuna jambo limetendeka usiku wa Jumamosi.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: