Tuesday, July 31, 2018

JEZI ZA MAZOEZI ZA TIMU YA MBAO FC NI SHIDA.


ABDALLAH CHAUS, MWANZA

Timu ya Soka ya Mbao fc ya jijini Mwanza imetambulisha jezi zao za mazoezi Rasmi watakazo zitumia katika msimu Wa 2018-2019,huku zikiwavutia mashabiki Wa timu hiyo kiasi cha kutaka kuzinunua na kuweka kumbukumbu ya picha na wachezaji Wa timu hiyo.


Jezi hizo zimemuonesha mdhamini Wa timu hiyo Gf Trucks and Equipment akiwa pekee mbele ya jezi hiyo huku wakiacha maswali juu ya mdhamini cowbell kuhusu udhamini wake na klabu hiyo.Akizungumza na FMG hii Afisa masoko Wa kampuni ya GF Trucks Kulwa Bindala alisema,kama wadhamini wakuu wameamua kubeba majukumu yote yanayoihusu klabu hiyo ikiwa ni kuleta jezi zenye Ubora na Mvuto kwa wadau Wa Soka huku akiahidi kushasha jezi nzuri zenye ubora kwa msimu huu 2018-2019.


Hii inakua ni mapema sana kwa timu hiyo kupatiwa jezi za mazoezi huku wadau wengi Wa soka wakiwa na hamasa na hamu ya kutaka kuziona jezi za msimu kutokana na kuvutiwa na uzuri Wa jezi za mazoezi

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: