Wednesday, July 25, 2018

JENERALI MABEYO AWATAKA WANANCHI KUJENGA TABIA YA KUPIMA AFYA ZAO

Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo amewataka wananvhi kupima afya zao mara kwa mara ili kunusuru vifo vya ghafra kutokana na wengi kutokuwa na utamaduni huo, huku akisisitiza watu kuwa na uzalendo wa kujitolea kwa taifa lao kama askari waliopigania taifa hili wanaokumbukwa hivi leo kama Mashujaa.

Jenerali Mabeyo amayasema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa ambayo ililenga upimaji wa bure kwa magonjwa ambayo sio yakuambukiza, huduma hiyo itatolewa mpaka siku ya Jumamosi katika viwanja vya Mashujaa mnazi mmoja.

Katika upimaji huo huduma zitakazo tolewa ni Upimaji wa Kinywa, Mama na mtoto, Ukimwi pamoja na Uwiano wa uzito.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: