Tuesday, July 24, 2018

INTER MILAN KUVUNJA REKODI USAJILI WA MESSI

Klabu ya Inter Milan imeamishia rada zake nchini Hispania wakitaka kufanya usajili wa kutisha, usajili utakao tikisa dunia, ambapo rada za klabu hiyo zinalenga kumsajili nyota wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi katika dirisha la usajili msimu huu.

Inter imefikia uwamuzi huo kumfukuzia nyota huyo, baada  siku chache kupita klabu ya Juventus ilipo amua kumsajili nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Inter wamesema wako tayari kutoa dau lolote lile ambalo wakala wa mchezaji huyo atalitaja, mashabiki wa timu hiyo tayari wameandika katika mitandao ya kijamii kuwa wanasubiri kwa hamu usajili wa nyota huyo.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: