Monday, July 9, 2018

HATUWAOGOPI ENGLAND - ZLATKO DALIC

Kocha wa wa timu ya Taifa ya Croatia Zlatko Dalic amesema kuwa kikosi chake tayari kimefanikiwa kumzuia Messi hivyo kinaweza kumkabili nyota wa tmu ya Taifa ya England Harry Kane Jumatano katika mchezo wa nusu fainali.

Dalic amewataja Kane na Raheen kuwa ni wachezaji tishio kwa timu ambayo haina udhaifu. Lakini tunaamini uwezo wetu , alisema "Hatuwaogopi England."

Kane ni mfungaji bora na sio rahisi kumzuia lakini tuna mabeki wa kati, tulifanikiwa kumzuia Messi na Eriksen kwa hiyo tuna matumaini ya kumzuia Kane.

Kocha huyo wa miaka 51 ambaye ameiongoza timu hiyo ya Taifa tangu Oktoba aliulizwa kuhusu uwezo wa timu ya England pamoja na udhaifu lakini akasema "siwezi kusema kuna udhaifu wako nusu fainali, hilo tu linasema kila kitu.

Kocha huyo ameongeza kwa kusema kuwa "Walionyesha kutoka kwa michezo ambayo nimeitazama kuwa wanacheza mpira na wana mbio sana, nafikiri kuwa Reheen Sterling ni mchezaji muhimu sana kwa sababu anambio sana na akiungana na Harry Kane ni hatari sana".

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: