Thursday, July 26, 2018

GEITA GOLD SPORTS KUKAMILISHA USAJILI WAO USIKU HUU KWA KISHINDO

Timu ya Geita Gold Sports ambayo imerejea upya baada ya Ukimia wa Muda, imepanga kukamilisha usajili wake usiku huu kwa Kishindo.

Akizungumzia na Famara News Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Seif Kulunge amesema kuwa Geita imepinga kuja na kishindo Kikubwa ambacho kitatikisa Nchi Nzima.

"Najua watu hawajui kwanini tumechelewa kukamilisha Usajili, ila niwaambie wasubiri kishindo ambacho hawajahi kukiona katika Soka Nchini hapa"

Kulunge amesema kuwa Geita Gold Sports ni ile ile kama ilivyokuwa zamani na Kikubwa wamejipanga kimbinu kuhakikisha wanacheza kupanda ligi Kuu maana uwezo wanao. 

Aidha amezitahadharisha timu zote kwa Ligi daraja la Kwanza na timu zote zitakazokutana Nazo kwenye Kombe la Shirikisho wajiandae maana wamerudi kwenye Soka kwa Makusudi na si Vingine.

Kuhusu Mdhamini wao Mgodi WA GGM Kama wako nao Kama zamani, Kulunge amesema hilo liko kwenye Mchakato atalitolea maelezo baada ya kukamilisha Usajili Usiku wa leo. 


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: