Wednesday, July 11, 2018

GARI LA SERIKALI LAKAMATWA NA KILO 800 ZA MIRUNGI

Gari la kubeba Wagonjwa (Ambulance) ya Hospitali ya Wilaya ya Tarime imekamatwa ikiwa imebeba Shehena ya kilo 800 za dawa za kulevya ambazo ni aina ya Mirungi.

RPC wa Mara amethibitisha kukamatwa kwa gari hilo na watu wawili, huku akisema gari hiyo ilikuwa ikitoka Mwanza kwenda Wilayani Tarime.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima amesema gari hilo lilikamatwa jana Julai 10, Wilayani Bunda.

"Dereva wa gari hilo aliitwa kwa ajili yakufanya kazi ya kubeba mgonjwa usiku wa jana lakini alisema yuko mbali na gari halina mafuta" Amesema Malima.

Pia Malima amesema dereva alitakiwa kumsafirisha mgonjwa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: