Friday, July 27, 2018

Diamond akiri kuzuiwa na Basata uwanja wa ndege

Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amesema kuwa alilazimika kusubiri masaa tisa ili kuendelea na safari yake baada ya kuzuiwa katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa kutokuwa na kibali cha Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) cha kufanya shoo nje ya nchi.

Diamond alitakiwa kuondoka saa 3 asubuhi lakini alisubiri hadi saa 11.

Siku ya jana mwanamuzi huyo alikuwa akielekea  katika visiwa vya Madagascar na Mayote ambako atafanya shoo yake leo Julai 27 na 28.

"Nikweli siku ya jana msanii wangu alikumbana na mkono wa Basata akiwa uwanja wa ndege, kwakuwa tulikuwa tumeisha lipwa hela ya watu ilibidi tukashughulikie kibali haraka ili aweze kuondoka nchini"Amesema Meneja wa mwanamuziki huyo Babu Tale.

Hata hivyo aliilaumu Basata kwa kushindwa kuweka kanuni zao wazi ili wasanii wazijue badala ya kuwasubiri wakosee ili wawachukulie hatua, nabadala yake amewataka wawe wazi ili wasanii waweze kufata kanuni hizo ili kuepusha mzozo.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: