Wednesday, July 11, 2018

CRISTIANO RONALDO AIKACHA KLABU YAKE YA REAL MADRID RASMI

Klabu ya Real Madrid tayari imethibitisha kuwa mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo amejiunga na Klabu ya Juventus ya nchini Italia.

Kwa taarifa zilizotoka zinasema kuwa klabu zote mbili zimefikia makubaliano ya malipo ya Pauni Milioni 105 kwa nyota huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 33.

Cristiano Ronaldo anaondoka Real Madrid akiwa ni mshindi wa tuzo ya Ballo d' or mara tano huku akiwa ameitumikia klabu hiyo kwa misimu tisa.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: