Friday, July 27, 2018

COASTAL UNION YAKAMILISHA USAJILI WA MWANAMUZIKI ALIKIBA

Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga umethibitisha kukamilisha usajili wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Akizungumza na kipindi cha michezo cha Sport HQ kinachorushwa na EFM Radio, Mwenyekiti wa timu ya Coastal, Steven Mguto amekiri kukamilika kwa usajili huo siku ya jana ambapo dirisha la usajili lilifungwa.

Uongozi wa klabu hiyo umesema kuwa imemsajili mwanamuziki Alikiba wakiamini kuwa watanufaika naye kutokana na umaarufu wake hivyo watu wengi watataka kumuona uwanjani, lakini pia atakuwa chachu hata kwa vijana wengine kushiriki kwenye michezo.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: