Monday, July 23, 2018

COASTAL UNION KUMNASA ALIKIBA

Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga umethibitisha uwezekano wa kukamilisha usajili wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, kwa ajili ya kuichezea timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Alikiba kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Mvumo wa Radi ambao unafanya vizuri katika vituo mbali mbali vya habari, msimu ujao anaweza akaonekana katika mechi kibao za ligi akicheza kupitia klabu yake ya Coasta Union.

Klabu ya Coastal Union imethibitisha kupitia kwa Mwenyekiti wa timu hiyo, Steven Mguto kuwa wapo kwenye mazungumzo na msanii huyo ili kupata huduma yake ya kuichezea klabu hiyo ya Coastal Union.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: