Wednesday, July 11, 2018

BEKA FLAVOUR AMCHANA MAKAVU ASLAY

Msanii wa muziki wa BongoFleva alimaarufu kama Beka Flavour amefunguka na kumtaka mwanamuziki mwenzake ambaye wamewahi kufanya kazi pamoja wakiwa kama kundi Aslay kuongeza nguvu na maarifa kwenye muziki wake ili aweze kufika mbali zaidi huku akimsihi aachane na masuala ya kiki za mitandaoni.

Beka amesema hayo baada ya kupita siku kadhaa tokea Aslay alipo achana na Mama watoto wake na kuamua kuweka wazi penzi lake jipya mitandaoni, ambapo jambo hilo wengi wameliona kama ni kiki ili kusudi aendelee kuzungumziwa sana na watu.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: