Tuesday, July 24, 2018

ASKARI WALIOHUSISHWA NA MAUAJI YA AKWILINA HATIMA YAO YAJULIKANA

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa ameweka wazi kuhusu askari waliokuwa wanashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) Akwilina Akwilin kuwa walikwisha achiwa huru kutokana na upelelezi kuonesha hawakuhusika na mauaji hayo.

Akwilina ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) aliuawa kwa kupigwa risasi wakati Jeshi la Polisi likiwatawanya waandamanaji wa CHADEMA, eneo la Kinondoni Jijini Dar es salaam waliokuwa wakielekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho.

"Ni kweli askari walishikiliwa ili kufanya uchunguzi katika mauaji yale, na mazingira ya kifo yalielezwa vizuri. Upelelezi ulionesha Askari hawakushiriki kwenye mauji hayo ila kilichosababisha ni maandamano haramu amabayo yalisababisha watu kukusanyika na vurugu zikatokea milipuko ya risasi ambayo ilipelekea tukio lile kutokea. Wale askari walitoka kutokana na jalada lilipopelekwa kwa mwanasheria ilionekana kuna udhaifu ndiyo maana hawajashtakiwa" Amesema Kamanda Mambosasa.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: