Sunday, June 10, 2018

YANGA NA SIMBA KWELI NI NDUGU?


Na Mandala J.

Mwenyekiti wa Yanga ameendelea kuwa ndugu Manji na uchaguzi kwa mujibu wa Waziri Harrison Mwakyembe ni kwamba Yanga wanapaswa kufanya uchaguzi mwaka 2020 kama nilimsikia vizuri na sasa ni mwaka 2018.

Yanga wanahitaji mabadiliko kwa maana ya kwamba wanahitaji mfumo mpya wa hisa kwa kufuata kanuni ya serikali ya 50+1 kubakia kwa wanachama na 49% kwenda kwa wawekezaji hapa sio muwekezaji ila wawekezaji kama Sheria za Baraza la Michezo inavyoeleza. Hapa ndio tunapata tafsiri sahihi kuwa sheria inasema wawekezaji   kwa tafsiri ya kwamba inafahamika ya kuwa hisa nyingi zinabakia kuwa kwa klabu na sheria imetamka kuwa 
" 18A-(1) Vyama au vilabu vya michezo vilivyoanzishwa na wanachama vikiamua kuuza hisa zake vinapaswa kutenga asilimia hamsini na moja kwa ajili ya wanachama wake na asilimia arobaini na tisa kwa wanaotaka kununua.."

Kumbe zile asilimia 49% zinaweza kugawiwa kwa wawekezaji wasio wanachama au wanachama wanaotaka kuwekeza ila zile 51% ni kwa ajili ya wanachama.

Subiri niendelee kusoma sheria hizi maana napata kuwaza kuwa kama mwanachama anakuwa na haki mbili katika kitu kimoja kuwa atawekeza na pia ni mwanachama atakuwa na haki ya kununua pia hisa zile za wanachama.

Ukiangalia hapa unapata namna ya kufikiri juu ya Manji kuendelea kuwa mwenyekiti na huku akitarajiwa kuwa muwekezaji maana uchaguzi unapaswa kufanyika mwaka 2020 , nasubiri kuona atapewa hisa zote au zitauzwa kwa namna kama ambavyo sheria inaruhusu kuwa na wawekezaji zaidi ya mmoja kwenye 49% ya hisa. Mi si mtaalamu wa sheria ila ukisoma kwa maana ya mwanzo utaona ninachokiona.

Ndio maana baada ya mkataba wa Simba na Mo tunasema sio sawa kwake kupewa uenyekiti kwa maana ya kwamba ni mwanachama na pia  ndie muwekezaji mkuu kwa hisa 49% na kwa namna ilivyo si sawa kwakuwa mwenye hisa nyingi amebakia kuwa Simba.

Hebu angalia hili upande wa pili wa Yanga ambao bado muwekezaji wao mtarajiwa ndie mwenyekiti pia hapa kutakuwa na conflicts of interests kubwa sana cha msingi nadhani kosa hili serikali wanaliona na wanalifanyia kazi pia. Suala kubwa hatukatai kuwa na wawekezaji na tunawahitaji sana sana kwa Mpira wa sasa na kikubwa ni kwamba tuliacha muda utuambie na umetuambia kuwa ni wakati wa kuwekeza kwenye mpira. 

 Lakini suala la mtu kuwa na hisa chache na kupewa uongozi wa juu kabisa sio sawa pamoja na kuwepo na hitaji la uwekezaji na sio kigezo cha kuharibu hata taratibu kuharakisha uwekezaji kama Simba walichofanya cha kupitisha mabadiliko ya katiba bila kupitia mkutano mkuu wa mwaka  wa klabu na kutumia mkutano mkuu wa dhalura ambao huwa na agenda moja tu   siku ile nakumbuka kama kulikuwa na agenda zaidi ya moja au ndio busara zilitumika kwani kwa mujibu wa katiba ya Simba  ibara 19-1 mkutano mkuu wa mwaka ndio wenye mamlaka ya kurekebisha katiba na sio mkutano mkuu wa dharura ulio katika ibara 22. Na wenye mamlaka ya kurekebisha katiba na kanuni zake ni wanachama kupitia mkutano mkuu wa wingi wa 50+1 ibara ya 27-2. Haya yalikiukwa kwa kuharakia uwekezaji ambao kila mmoja anautaka tukumbuke kuwa kuna wakati ukiwa na huhitaji wa kitu kwa kiwango kikubwa ufanisi hupungua nachelea kusema hivyo.

Tukumbuke tunayoyaaona baadae yana madhara yake makubwa japo tunayapuuza na kuona tu tunahitaji mabadiliko na kwenda katika mfumo wa hisa kwa kufuata utaratibu au kutofuata utaratibu.

Kama Yanga mwenyekiti wao atakuwa Manji na apewe uwekezaji kwa kupewa asilimia 49% itakuwa sio sawa na kibaya zaidi utakuta mwanachama au mpenzi anakuambia ikiwezekana wapewe kabisa timu kwani miaka 80+1 ya hizi timu hakuna chochote kilichofanyika jambo ambalo sio kweli kwani hivi vilabu vina msingi mkubwa sana na baadhi ya vitu kama viwanja na majengo ambavyo ni dhahiri kuna kitu hizi timu zimefanya, japo aina ya viongozi waliopita walikuwa na malengo binafsi na sio malengo ya timu.

Yanga tunataka kuona wanafanyaje? Kikubwa wanafuata taratibu zao kama katiba yao inavyosema kuepuka migogoro isio na tija mbele ya safari tukumbuke hii hali tunayoiona ya kuhitaji sana mabadiliko kuna kipindi mabadiliko tutayazoea na kuanza kufikiri vizuri na hapo hatari hizi zitafumuka kwa sasa yawezekana tunaona bora liende na uhitaji kuwa mkubwa na kutufanya tushindwe kufikiri kwa kina. 

Yanga wanaamuaje kuhusu hili ila wakumbuke njaa sio kigezo cha kuifanya Yanga isiwe Mali ya umma na uwekezaji unaofanywa uwe kwa ajili ya kulinda Mali ya umma.

Karibuni sana Yusuph Manji na MO katika sura mpya ya kuwekeza katika vilabu hivi na uhutaji wenu wa vilabu hivi ni tija kwa vilabu vya Simba na Yanga.

Hapa najaribu kuangalia linapotokea suala la kimaamuzi katika uwekezaji au kutokuelewana katika maamuzi kati ya muwekezaji na klabu huku mwenyekiti au rais wa klabu ndie muwekezaji itakuwaje? Kuwa mwanachama na pia kuwa muwekezaji kuna tatizo naliona kama ninavyoliona kuwa rais wa klabu huku wewe ni mwanachama na una hisa chache dhidi ya klabu  kuna tatizo pia. Mchakato wa uwekezaji wa klabu ya Simba unafunzo kwa mchakato wa uwekezaji pale Yanga. Kikubwa kuna haja ya kuona namna gani sahihi ya kufanya mapema ili tuende na michakato iliobora na sawa kabisa kwa maendeleo ya mpira wetu. 

Huu ni mtazamo wangu juu ya Mali za umma.

#YangaSimbanimaliyaumma.
+255659797279
+255620639779

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: