Saturday, June 9, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AAGIZA SOMO LA MICHEZO KUANZA KUFUNDISHWA NGAZI ZA AWALI HADI CHUO KIKUU.

Mkurugenzi Nyanza Bottling Company Limited  Christopher Gachuma akisalimaina na Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

NA OSCAR MIHAYO, MWANZA

KUTOKANA na Tanzania kuendelea kushuka kwa viwango  vya soka kimataifa, Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ameagiza somo la Michezo lianze kufundishwa kuanzia Ngazi ya awali hadi Chuo Kikuu.

Hayo ameyaeleza leo uwanja wa CCM Kirumba alipokuwa anafungua mashindano ya Umoja wa shule za Sekondari na msingi Umeseta na Umitashumta kitaifa inayofanyikia katika viwanja vya chuo cha walimu Butimba na Shule ya Sekondari Nsumba.

Mh, Majaliwa alisema ni vyema sasa masomo hayo ya Haiba ya Michezo kufundishwa kwa ufasaha ikiwa na Halmashauri kuajili walimu wenye taaluma ya Michezo ili kuweza kuleta tija kwa taifa.

Aidha Majaliwa ameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinatenga bajeti ya Michezo kwa kila shule ikiwa na kutoa vifaa sahihi sahihi vya Michezo kwa shule za Sekondari na Michezo ili kuweza kupunguza changamoto zinazokabili sekta hiyo.


Mheshimiwa Majaliwa pia aliwaonya walimu wanaleta mamluki kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ya kitaifa kuwa wakibainika sheria kali zitachukiliwa dhidi yao ikiwa na kuwataka kutumia wanafunzi ambao wako shuleni.

Pia amewataka wanafunzi kuhakikisha wanatendea haki nafasi waliyoipata kwa kuonyesha vipaji vyao halisi kama njia ya kujiandalia ajira kwenye soko la badae kutokana na uwepo wa maskauti wanaotafuta U-20 kwa ajili ya kuwalea kwenye timu zao za Simba, Yanga na Azam.

Awali akisoma risala Naibu Katibu Mkuu elimu Ofisi ya Tamisemi Joseph Kakunda alisema mashindano hayo kwa Mwaka huu yanashirikisha wanafunzi 3680 kutoka Mikoa 28 ya Tanzania Bara na visiwani.

Kakunda alisema lengo la mashindano hayo ni kuimarisha taaluma na ujuzi, uzalendo, umoja na mshikamano, afya ukakamavu ikiwa na ujasiri kati ya walimu na wanafunzi pamoja na kujenga utaifa.

Mashindano hayo yamefanyika mara tatu mfululizo jijini hapa ikiwa Bingwa wa jumla mwaka jana ulikuwa Mkoa wa Dar es Salaam na mshindi wa pili akiwa Mwanza.
  Wanafunzi wa Umiseta mkoa wa Simiyu wakipita mbele ya Mgeni Rasmi Kassim Majaliwa leo katika Uwanja wa CCM KIRUMBA.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: