Tuesday, June 5, 2018

WAZIRI APIGA MARUFUKU TRILION 1.5 KUJADILIWA NDANI YA BUNGE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama amewataka Wabunge kutojadili suala la Trilioni 1.5 ndani ya bunge kutoka kwenye ripoti ya CAG, hadi kamati ya PAC itapowasilisha ripoti yake.

Waziri Jenista ametoa kauli hiyo leo Bungeni baada ya Mbunge wa Kibamba John Mnyika kusimama na kuihoji Serikali kuhusu fedha hizo ambazo ziliacha gumzo kubwa kwa umma na wanasiasa baada ya ripoti ya CAG kutolewa mapema mwa mwezi April mwaka huu.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: