Tuesday, June 5, 2018

WALIMU WAKIUME WATAKIWA KUPIMA DNA

Waalimu na wafanyakazi wa jinsia ya kiume katika shule ya Upili ya Moi Girls Nairobi watapimwa DNA ili kumbaini mtu aliyehusika na ubakaji wa mwanafunzi katika shule hiyo hiyo June 1, upimaji huo utamuhusisha kila mtu wa jinsia ya kiume aliyekuwepo siku hiyo.

Taarifa kutoka Kenya zinasema kuwa tayari maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha uhalifu na mkemia wa serikali hapo jana Jumatatu walichukuwa sampuli za wafanyakazi wanane wa shule hiyo ili kufanyiwa ukaguzi wa maabara.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: