Tuesday, June 5, 2018

SINGIDA UNITED YAFATA NYAYO ZA SIMBA

Klabu ya Singida United imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-2, hiyo ni baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare tasa 0-0.

Kwa matokeo hayo Singida inakuwa ni timu ya pili ya Tanzania kufuzu hatua hiyo ya nusu fainali baada ya Simba SC siku ya jana kutinga hatua hiyo ya nusu fainali kupitia mikwaju ya penati.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: