Tuesday, June 12, 2018

SIMBA SC NJIA MNAYOITAKA YA UWEKEZAJI INA MIBA.Na Mandala J.

Naomba kutoa mtazamo wangu juu ya kinachoendelea katika vilabu vyetu vya Simba na Yanga ila kwa Leo ntaegemea kwa yanayoendelea katika klabu ya Simba maana ya Yanga bado.

Nakubaliana na uongozi wa Simba katika harakati zao za kuifanya Simba iwe timu bora na ya ushindani hapa Tanzania , Africa na duniani pia wanafanya kazi nzuri sana na ndio maana wameamua kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu yao na kukubali muwekezaji kuwekeza yaani mwanachama wao, Mtanzania mwenzetu ndugu Mo, ni suala la kushukuru kwa dhamira yake ya kuona fursa na kuamua kuitumia kwa manufaa yake na klabu pia. Alipotaka kuwekeza kwa 51% na kushindikana na serikali kuingilia kati lilikuwa wazo bora na nzuri lengo likiwa ni lile lile yaani maendeleo ya mpira wetu na ulinzi wa Mali ya umma.

Mfumo wa 50+1

Huu ni mfumo ulioasisiwa Ujerumani baada ya DFL kuona mbona bei za ticket za uwanjani zinashuka , mahudhurio viwanjani ni madogo ilikuja kuonekana kuwa hakuna mahusiano ya karibu kati mashabiki au wanachama wa klabu na klabu na njia ya kitaalamu ikawa kuja na mfumo wa 50+1%. DFL wakaja na wazo kuwa timu yoyote inayoshiriki Bundesliga itapaswa kuwa katika mfumo wa 50+1% na ikawa ngumu tu kwa Bayern Leverkusen na Wolfsburg ambao walikuwa katika mfumo mwingine na hata mwaka 2009 Hannover walipotaka kuturn over (kwenda kinyume na kwanini hii) walikataliwa pia.

Malengo yalikuwa ni nini?

Malengo yalikuwa klabu zitabakiwa kuwa Mali ya umma na kuachana na wawekezaji ambao hufikiri zaidi faida kuliko matakwa ya mashabiki maana halisi ya mpira sio faida tu bali kuleta furaha kwa wananchi walio wengi.

Pia ilikuwa kulinda utamaduni wa kidemokrasia yaani maamuzi yafanyike kwa wengi wape na wachache wasikilizwe ili kufikia lengo la kuleta furaha na amani kwa wananchi walio wengi nchini Ujerumani na kikubwa kuyaacha maamuzi ya juu ya klabu mikononi mwa wanachama na wapenzi wa timu husika.

Hata CEO wa Bayern Munich ndugu Karl Heinz Rummenigge alipotoa wazo la kila timu kutafuta mwekezaji kwa mfumo wake alikataliwa na lengo ilikuwa kuwa sio Wawekezaji wote wana tabia kama za Roman Abromovich anaetaka ushindi kwa timu yake kutimiza furaha ya moyo wake.

Faida za mfumo.

Wanachama kutoichoka timu na kuwa na utawala juu yake maana kitendo cha kuwa na hisa kwa mwanachama ina maana kuwa wanakuwa ni wazalishaji wakubwa maana mwisho wa siku faida kubwa inabaki kwao na kwa timu yao na haitaenda kwa muwekezaji maana wakichanganya umiliki wao wa hisa kwa maana ya kupata gawio wanakuwa na pesa nyingi ambazo zinarudi kwa klabu yao kwa njia ya kununua ticket bidhaa za timu hivyo kuifanya timu yao kuwa na nguvu kifedha na kuamua njia ya aina ya kuleta furaha na maendeleo ya timu yao na kuziongezea kipato na kufanya mashabiki au wanachama kuwa karibu na timu na kuwepo uwanjani kwa michezo ya timu yao kuliko kuwa na utawala wa mtu mmoja na hii ukiangalia kwa namna nyingine ni kulinda vilabu vikubwa kuendelea kutawala maana ndio vyenye wanachama wengi na kuendelea kuwa na jina zuri la biashara( Goodwill). Hata serikali yetu ililiona hili na kuamua kuwa na mfumo wa 50+1 % kwa maana ya serikali kuamua hivyo ina maana ya kwamba vilabu vyote vinavyotaka wawekezaji kwani inatamka wanaotaka kununua lazima iwe 50+1% kwa wanachama. Rejea Sheria za Baraza la Michezo la Taifa 18A (1).

UWEKEZAJI SIMBA SPORTS CLUB.

Mtazamo wangu napenda kuuweka wazi kama mwananchi wa kawaida sana na mfuatiliaji wa mpira wa miguu Tanzania.  Sipingi uwekezaji wa Mo kabisa ni kama vile sikupinga ukodishwaji wa Yanga wakati ule maana ilikuwa ni ukosefu wa utashi wa kufikiri tu ndio ilikuwa sababu.

Simba na Mo wamegawana hisa yaani 51%(50+1)  kwa 49% na kufanya Simba kuwa na hisa nyingi kuliko Mo. Na hapa angalia umiliki wa hisa katika timu ya Bayern Munich kama mfano kwani ndiko mfumo ulikotoka kuwa ni 75% kwa Bayern Munich (50+1) na wamiliki wengine akina AUDI, Adidas na Allianz kugawana 25% kwa 8.33% kila mmoja wao kama kampuni ( 49% kwa wanaotaka kununua kwa maana wawekezaji wengi na ndio sheria yetu kama muongozo inavyosema hapa Tanzania na kwa Ujerumani wao Bayern Munich wameziuza wa wawekezaji na sio muwekezaji) na hisa za Bayern Munich Ag kuwa zinamilikiwa na wanachama japo wanachama pia hawajawekwa wazi lakini mgawanyo wa hisa ni kati ya Bayern Munich , Audi, Adidas na Allianz na kiongozi wa juu anatoka katika klabu ya Bayern Munich na sio kwa mwanachama mwenye hisa nyingi ila kwa kampuni yenye hisa nyingi. Faida zake nimeeleza hapo juu.
Simba wanachofanya ni makusudi yasioendana na mfumo halisi na matakwa halisi ya mfumo wa uendeshaji kwa maana ya kwamba 50+1% pamoja na kukiuka katiba ya mwaka 2014 ili kuharakia mabadiliko rejea mkutano wa dharura kupewa mamlaka ya kubadili katiba kuliko mkutano mkuu wa wanachama ukiwa ndio wenye mamlaka ya juu katika hili hapa watu wamefunika kikombe mwanaharamu apite.  
Kumpa urais MO ni kutokuutendea haki mfumo Na muundo mzima wa uendeshaji katika mfumo huu kwa maana ya kwamba Simba ndio wanaopaswa kulinda bidhaa yao na MO anapaswa kulinda pesa zake na hapa mgawanyo wa hisa na utawala si kati ya wanachama ila ni kati ya Mo na Simba .
Kubadili katiba kwa ajili ya kutimiza takwa la Mo kuwa rais au mwenyekiti ni usaliti mkubwa sana na kibaya unaona mambo yavyoenda haraka ndio mtu unakosa uaminifu na kinachoenda kutokea huku kikiwa na madhara makubwa mbele ya safari kwa maana ya kwamba wanachama kupokonywa maamuzi juu ya klabu yao na kuifanya klabu ya Simba kama Mali ya umma kuwa Mali ya mtu binafsi kimatendo. Leo inaweza isionekane kwa jicho la kawaida na kwa nguvu ya vuguvugu , niamini tatizo hili litaibuka mbele ya safari kwa uwazi kabisa na watu watanyosheana vidole.

Swali hapa ni kuwa MO akiwa mwenyekiti kwenye kikao cha board maamuzi yataegemea wapi? Na hapa panatoa mwanya wa rushwa katika maamuzi magumu yanayohusu timu ya Simba na kufanya timu kupokonywa kiujanja ujanja.

Nashindwa kuelewa akina Mwina Kaduguda, Ismail Aden Rage, Mzee Dalali, akina Julio hili hamlioni nyie au Mimi nafikiri na kuona tofauti naombeni kuelimishwa nielewe ila naona kama viongozi wa Simba wanataka kutusaliti wafuatiliaji wa soka au mambo ya mpira Tanzania.

Kwanini MO ang'ang'anie kuwa rais ili hali anajua mwenye hisa nyingi ndio mwenye sauti kuu, kwanini anataka kuwanyang'anya simba haki yao sababu ya njaa yao au sababu ya nn? Maneno ya Jerry Muro na pesa za Yusuph Manji zilizowatesa katika misimu sita iliopita na kuchoka kabisa. Hawa Simba tuliwauliza  walifanyaje kupata thamani ya 20bn limekuwa swali na Leo wanataka kufanya kosa lingine kiufundi kwa manufaa ya nani?

Viongozi wa Simba wamekuwa watu wanaokosa integrity kwa mambo ya wazi kabisa hawa viongozi waliopo madarakani hata ukiwauliza zile pesa za OKWI ziko wapi au ilikuwaje ? zimekosa majibu , muda wao unaelekea kuisha ndio wanaharakisha kupitisha haya , unapata ukakasi na unapata wapi? Amani juu yao kwa kuendelea kuzua maswali juu ya kinachofanyika huku nyuma kukiwa na historia isio na integrity ( Uaminifu) na hili ukiwa kiongozi tu ukishukiwa kwa baya lolote unakosa integrity na hawa kwa kuibua maswali haya tunawaaminije?

Simba warudi katika maana halisi ya mfumo wa 50+1 waachane na kumpa urais MO maana kutakuwa na hasara kubwa mbele ya safari japo sasa kunaonekana kuko poa na yanayokuja yanafurahisha, Si sawa tusikubaliane na hili kabisa pawepo na uelewano sahihi ya kuendelea kuifanya Simba kuwa Mali ya umma labda kama hilo linaondoka.

Kuna vitu vinatakiwa kuwa wazi pamoja na utoaji wa hizo pesa na mambo mengi ni heri kabla ya uongozi huu haujatoka madarakani kuwepo na Audited Financial Statement report ili kujenga Integrity juu viongozi hawa.
Sipingani na uwekezaji unataka kufanya nauhitaji sana tena kuliko na ndio maana nilikuwa tayari hata Yanga wakati ule wakodishe timu kwa mkataba wa maslahi ili kutoa namna ya upatikanaji wa faida kwa Yanga cooperation ltd lililokuwa lengo la Yanga kama klabu kuanzisha kampuni hiyo.

Je? Kupewa urasi hisa 49% dhidi ya 51% ni sawa.

+255659797279
+255620639779

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: