Tuesday, June 5, 2018

SIMBA NA YANGA USO KWA USO KAGAME CUP

Mahasimu wakubwa wa mchezo wa soka Tanzania, Simba na Yanga zimepangwa kundi moja kwenye michuano ya Kombe la Kagame Cup inayotarajiwa kuanza Juni 28 hadi Julai 13, 2018.

Wababe hao wamepangwa kundi C ambapo zimejumuishwa na klabu nyingine za St. George kutoka Ethiopia na Dakadah ya Somalia.

Bingwa wa michuano hiyo atapata Dola $30,000 sawa na Tsh 68.4 na mshindi wa pili atapata Dola $20,000 ambazo ni sawa na milioni 45 huku 45 huku mshindi wa tatu ataondoka na Dola $10,000 sawa na milioni 22 za kitanzania.

Michuano hiyo itafanyika nchini Tanzania na michezo yote itarushwa live kupitia Azam TV.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: