Tuesday, June 5, 2018

NSAJIGWA ANG'ATUKA YANGA SC

Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga SC, Shadrack Nsajigwa ametangaza kuachana na wanajangwani hii leo baada ya kumaliza mkataba wake aliosaini kuitumikia timu hiyo.

Nsajigwa amethibitisha hayo wakati alipokuwa akizungumza na eatv.tv mchana wa leo ili kupata uhakika juu ya taarifa ambazo zilikuwa zimezagaa kila kona kuhusu kuachana na klabu hiyo.

"Hizo taarifa ni zakweli kabisa na nimechukua maamuzi hayo baada ya mkataba kuisha muda mrefu tokea siku Ligi Kuu Tanzania Bara ilipomalizika kwa msimu wa mwaka 2017/18" Amesema Nsajigwa.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: