Tuesday, June 5, 2018

NKURUNZIZA KUPOKEA KATIBA MPYA

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anatarajiwa kuipokea Katiba mpya ambayo taanza kutekelezwa siku ya Alhamis ambayo inatajwa kuwa itageuza mambo mengi kwenye taifa hilo, lakini pia kutoa fursa kwa Rais kuweza kuwania uongozi wa nchi hadi mwaka 2034.

Taarifa kutoka Ikulu ya Burundi zimethibitisha kuwa sherehe za utiaji sahihi kwenye katiba mpya na kuitambulisha kwa raia zitafanyika katika mkoa wa kati wa Gitega eneo la Bugendana ambako huko ndiko kulikozinduliwa rasmi mchakato wa katiba.

Katiba hiyo inaanza kutekelezwa wakati mazungumzo ya amani yakiwa yamekwama baada ya serikali kukataa kuketi meza moja na wapinzani.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: