Thursday, June 7, 2018

MWAREDDA KUTOA BIMA YA AFYA KWA MADEREVA NA MAKONDAKTA.

NA OSCAR MIHAYO, MWANZA

CHAMA Cha Madereva na Makondakta mkoani Mwanza (MWAREDDA) kinatarajia kutoa  Bima ya Afya kwa zaidi ya madereva na Makondakta 40 kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lengo likiwa kupamabana na changamoto wanazokumbana nazo pindi wanapokuwa wameugua ama kupata ajali.

Akizungumza na Famara Mwenyekiti wa MWAREDA Mujalifu Manyasi amesema zoezi hilo ni moja kati ya mipango ya chama hicho katika kujali afya za waendesha daladala na makondakta mkoani hapa  ikiwa unapodai haki zingine ni lazima uwe na uhakika wa afya yako kwa kuwa na bima ya afya.

Manyasi ameleza kuwa wamefikia hatua hiyo mara baada ya kukumbwa na changamoto za mara kwa mara pindi wenzao wanapokuwa wameugua hali ambayo huwalazimu kutembeza bakuli na mwisho kufariki kwa mgonjwa kabla ya kupatikana kwa pesa ya matibabu.

“Jambo hili limetutesa sana kwa kipindi kirefu na h ii ni kutokana na kutokuwa na mawazo chanya ya kukabiliana na tatizo hili lakini kupitia mpango huu nadhani tunaenda sasa kukomesha na kumaliza tatizo hili,’’alisema Manyasi.

Manyasi pia amewaomba wananchama wa umoja huo ambao ni zaidi 300 kukubali kuungana na wenzao kwa ajili ya kupata bima hiyo ambayo itawafanya kufanya kazi kwa kujiamini na kuwaongezea thamani ya mishahara kutoka kwa waajili wao.


Manyasi pia amewapongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kukubali kutoa bima hizo kwa kundi hilo ambalo lilikuwa limesahurika na kwa kuwapunguzia gharama kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo muhimu.

Kwa upande wake mjumbe wa umoja huo Florence Msilotwa Dereva wa njia ya Mecco amewapongeza viongozi kwa kuja na mwalobaini ambao umekuwa umewapa wasiwasi pindi wanapokuwa kwenye shuguli zao za kila siku.
Manyasi pia ameongeza kuwa Bima hizo zinatarajiwa kutolewa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu mwishoni mwa mwezi huu katika Stendi ya mabasi yaendeyo mikoni Buzuruga.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: