Tuesday, June 5, 2018

MBAO FC YAPATA KOCHA MPYA

Aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Lipuli FC ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Simba Amri Said, amejiunga na klabu ya Mbao FC ya Mwanza kama kocha mkuu wa kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2018/19.

Amri Said amechukuwa nafasi ya aliyekuwa kocha wa muda Fulgence Novatus, ambaye aliiongoza timu hiyo baada ya kuondokewa na aliyekuwa kocha wake Mkuu, Mrundi Etienne Ndayiragijje ambaye kwa sasa amesaini kuifundisha KMC ya Kinondoni.

Amri Said amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kuifundisha Mbao FC ya Mkoani Mwanza.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: