Friday, June 8, 2018

KIHOWEDE YAWAPATIA SEMINA WAZAZI JUU YA USAFIRISHAJI HARAMU.

Mratibu wa Shirika la Kihowede Lulu Makwale akitoa Elimu juu ya Madhara ya usajfirishaji haramu wa watoto kwa wazazi na walezi Mkoani Mwanza.
Wazazi na walezi kutoka Mkoani Mwanza wakifuatilia kwa makini mafunzo juu ya Elimu juu ya madhara ya usafirishaji haramu wa watoto.
NA OSCAR MIHAYO, MWANZA
SHIRIKA linalotetea Haki za Watoto na Wanawake Mkoani Mwanza (KIWOHEDE) limeendesha semina kwa wazazi na walezi 200 kutoka mkoani hapa ambao watoto wao wapo katika hatari ya kusafirishwa kwa njia haramu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo Mratibu wa shirika hilo Lulu Makwale, alisema watoto hao wako kwenye hatari kutokana na kuwa kwenye mazingira magumu na wengi wao wakiwa wameacha shule.
Lulu alieleza katika semina hiyo wazazi hao na walezi watakumbushwa juu ya majukumu yao ya msingi ikiwa na kuwa karibu na watoto wao na suala zima la malezi bora ili kumlinda mtoto na janga hili hatari.
"Tumeona tuanze kutoa elimu juu ya madhara wanakumbana nayo watoto  wanapokuwa wameingia kwenye usafirishwaji haramu kwenda mijini kwa minajili ya kufanya kazi za ndani ikiwa na ukatili wa kingono, kimwili, kiuchumi na kisaikolojia,"  alisema Lulu.
Lulu alieleza kuwa kutoa Semina hiyo kwa wazazi ni baada ya kufanya  utafiti na kugundua kuwa elimu juu ya usafirishaji haramu wa watoto bado ikiwa na wazazi kukimbia majukumu yao ya malezi  nakubakia kuwategemea watoto hao.
Alisema katika mradi huo kuna makundi mbalimbali ambayo yatafikiwa ikiwepo watoto 750 ambao wataokolewa katika hatari hiyo 100 kati yao ni a Kliume Na 650 ni watoto wa kike ambao watapewa malezi katika Kituo hicho kwa Mwaka Mzima.
Lulu pia alizitaja wilaya zitakazonufaika Na Mradi Huu Kuwa ni Nyamagana, Ilemela, Sengerema, Magu na Misungwi  zote za mkoani hapa.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: