Tuesday, June 12, 2018

KABILA LA WAHA MKOANI MWANZA WAANZISHA UMOJA WAO.

NA OSCAR MIHAYO, MWANZA
KUTOKANA na makaburi yaliyoko sehemu mbalimbali jijini hapa kujaa na kukosa sehemu ya kusitiri wenzao vizuri, Waha kutoka mkoani Kigoma wanaoishi Mwanza wameamua kuanzisha umoja wao wa kusaidizana kwenye magonjwa na misiba ili kusafirisha marehemu hadi Kigoma.
Akizumgumza na Famara Midea Group  Mtemi wa Umoja huo Edemes Kalimanzira  alisema umoja huo wenye wajumbe 27 una lengo la kuwakutanisha pamoja kuchangishana  kwa lengo la kusafirisha na kuzika nyumbani kwao kwa mila na desturi za waha.
“Mimi mwenyewe nilifiwa na wanangu wawili lakini ukienda kwa sasa nilipowasitiri makaburi ya umma huwezi kutambua kaburi ni hii imekuwa ikinipashida kwa watu wangu wa karibu wanaokuja na kutaka kwenda kutoa Baraka kwa wanangu kama mila zinavyohitajika, ” alisema Kalimanzila.
Bw. Kalimanzila aliongeza kuwa mapema mwezi wan ne walipata msiba wa ndugu yao Muha kutoka Kigoma na alikuwa hashirikiani na nzengo ya mtaa alipokuwa anaishi hivyo walipata shida sana kujichnaga na kumsafirisha hadi nyumbani kwao na ndipo kwa umaja wakaamua kuanzisha umoja huo.
Aidha alisema kwa sasa licha ya kuwa na mfuko mado wanahitaji mfadhili wakuweza kuwapatia usafiri wa kuzunguka kwa wenzao hasa majira ya usiku endapo mwanaumoja huo anapokuwa amepatwa na matatizo.
Alieleza kuwa licha ya kuwa wanaendelea kutunisha mfuko kwa kujichanga mfukoni lakini bado wanaangalia uwezekano wa kuwa na vitega uchumi endapo wataweza kupata msaada kutoka kwa wahisani au wanaoguswa na umoja huo.
Kwa upande wa mjumbe wa umoja huo Zebadayo Joseph alisema kabla ya kuwa shida sana ilipoikuwa ikitokea msiba ama matatizo ya kuugua ama kuuguliwa na mtu wako wa karibu hali iliyokuwa ikiwalazimu kutembeza  bakuri.
Aliongeza kuwa kwa sasa anaivunia kuwa na umioja unaokwenda kwa jina la “Abaha Tufashanywe” ikiwa na maana waha tusaidizane na kuwataka watu wengi kutoka kigoma kuungana kwa pamoja ili kuwa na nguvu kubwa zadi.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: