Friday, June 8, 2018

JAMII IMEOMBWA KUTUNZA MAZINGIRA NA USAFI ILI KUJIEPUSHA NA MAGONJWA MBALIMBALI.


Mwanza

Wafanyakazi Wanaojihusisha na Usafi Wa Barabara na Mitaro Jijini Mwanza Wamezungumzia Kuhusiana Na Mwitikio wa Usafi wa Mazingira Katika Jiji Hilo.

Hayo yamesemwa na Baadhi ya Wafanyakazi hao Kutoka Maeneo Tofauti tofauti Jijini Mwanza Wanaojighulisha na Usafi wa Barabara na kwenye Mitalo.

Wakizungumza na  Kwa Neema Fm Radio, Wafanya kazi hao Wamesema kwa sasa Hali ya Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza Inaendelea Vizuri Hii ni Kutokana na wakazi wa Jiji hilo Kuitikia Mwito wa Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira Kwakutotupa taka Hovyo.

Aidha Wafanyakazi Hao wamesema Zipo Changamoto Wanazokutana nazo Katika kazi zao Kama Vile Baadhi ya Watu kutofuata Utaratibu Ulio Mzuri Wa Utupaji Taka. 

Kwa Upande wao Wakazi wa Jiji Hilo Wameelezea kuhusiana na Uhifadhi wa Mazingira na Wamesema Kwasasa Wamehamasika Vyema Katika kuyatunza Mazingira,Hii ni Kutokana na Juhudi Zinazo Fanywa na Serikali na Wadau wengine wa Mazingira Ikiwemo Siku ya Mazingira Duniani Inayoadhimishwa Kila Ifikapo  Juni 5.

Hata Hivyo Wakazi Wote wa Mwanza Wametakiwa Kuyatunza na Kuyahifadhi Mazingira Kwani Mazingira Yaliyo Safi ni Sehemu ya Maisha Na Tuyatunze Mazingira ili Yatutunze.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: