Saturday, June 9, 2018

GOSHEN CHOIR KUTOKA MWANZA WAANDIKA HISTORIA MPYA.


Na Mwandishi Wetu, MWANZA
KWAYA ya Goshen kutoka la Goshen Inland Church Mwanza wameandika historia mpya baada ya kufanya uzinduzi mkubwa hivi karibuni katika Uwanja wa Shule ya Msingi wa Mabatini Mkoani Mwanza.

Uzinduzi huo uliofanyika tarehe 3 Juni Mwaka huu, ukishirikisha Kwaya zaidi ya thelathini uliwapa raha wananchi wa Mwanza kutoka vitongoji mbalimbali kupata upako kupitia nyimbo zao walizoimba.

Akizungumza na Website wa Famara News Katibu wa Kwaya hiyo Jacob Simba alisema kuwa Mungu amewashangaza kutokana na jinsi ilivyokuwa siku hiyo maana hawakuamini kilichotokea.

''Mungu ametupa heshima na Mungu ametukumbuka maana alichokifanya kwetu ni tofauti na jinsi tulivyokuwa tunawaza ila kwa neema yake ametustahilisha, tunampa sifa yeye mwenye nguvu na mamlaka yote''

Aidha amesema  baada ya kuzindua albam yake ya MUUJIZA WA TOBA ambayo iko mfumo wa DVD, kwa sasa wanaelekeza akili zao kwenye ziara za makanisa mbalimbali na mialiko waliyonayo ili kuwapa watu urahisi wa kupata DVD yao mpya ambayo iko madukani ikisambazwa na HMC kutoka Moshi Kilimanjaro.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: