Tuesday, June 5, 2018

GOLIATH: SINA OFFICIAL DESIGNER ILA IT'S OK!


Rapa Goliath ambaye ni zao jipya la muziki wa rap jijini Mwanza anayehit na wimbo wake wa "It's Ok" amefunguka kuwa suala la kuvaa kwake huwa halimuumizi kichwa sana kiasi cha kumfanya atafute designer.

"Bro mimi huwa najikuta tu naambiwa nipo ok, na ukweli ukiudadisi sina official designer anayesimama before the audience. So every appearance nafurahi kuwa real japo sometimes being real it doesn't simplify to achieve the success" amefunguka mkali huyo anayetoka mtaa mmoja na mkongwe Dudubaya.

Mapema jana alipokuwa akipiga story na mtangazaji Swaiba Tanzania "wakienyeji" kupitia Mdundo Bando ya 102.5 Lake Fm, amezungumzia picha zilizosambaa kwa kasi hivi karibuni zikimuonesha amevaa suti na mdada aliyevaa vazi la harusi (wedding dress) amesema
 
"Zile ni picha za kitambo kidogo, zilipigwa 2016 wakati nafanya video ya wimbo uitwao wife material.. Unajua watu ambao hawakuwa wanamjua Goliath ndio wamekuwa surprised na kuona ni kitu kipya kiasi cha kufikiri nimefunga ndoa kimya kimya au ni project mpya!"

Endelea kusikiliza wimbo wake "it's ok" aliomshirikisha Manengo na kufanywa na producer Hpol.

Kwa habari za uhakika usikose kutembelea https//:www.famaranews.com ndio chaguo sahihi.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: