Tuesday, June 5, 2018

BAADA YA UPASUAJI LISSU AIBUKA NA JIPYA

Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amefunguka na kuwashukuru watanzania wote kwa kuweza kumuombea na kutoka salama katika chumba cha upasuaji jambo ambalo anasema limempa matumaini makubwa yakupona kabisa.

"Hello wapendwa wangu nawasalimu wote kwa upendo mkubwa ile mbio ya marathon ya jana iliisha salama baada ya masaa saba. Sasa nimeingia kwenye hatua ya uponyaji, Mungu ni mwema amewawezesheni kuendelea kunipagania. Bila shaka ataniwezesha kwa kupitia kwenu kumaliza sehemu hii iliyobaki. Mungu awabariki sana na awaongezee mlikopungukiwa" Amesema Lissu.

Lissu ametoa neno hilo ikiwa imepita siku moja tokea alipomaliza kufanyiwa upasuaji ambao upasuaji huo ulikuwa wa 20 kwa Mbunge huyo.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: