Friday, April 20, 2018

UGONJWA WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI WATAJWA KUWA UGONJWA HATARI KWA SASA.

Mratibu wa Chanjo ya Saratani Amos Kiteleja ametoa maelekezo kwa Wanahabari katika Semina ya kuwajengea uwezo wa kufahamu kuhusu Virus vya Human Papiloma Virus.
Mwanahabari Willhelm Mulinda kutoka The Guardian akifuatilia kinachoendelea kwenye Semina.
              Nashon Kennedy kutoka Gazeti la Daily News.
                          Mafunzo yakiendelea kwa Wanahabari
 Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Silas Wambura akisikiliza maelekezo kutoka kwa Mwezeshaji.
                     Mwonekano wa Wanahabari Ukumbuni ulivyo
OSCAR MIHAYO
MWANZA

SARATANI ya shingo ya kizazi kwa wanawake imetajwa kuongoza kwa kusababisha vifo vingi hapa nchini , na virusi vijulikanavyo kama Human Papillomi (HPV).
 
Hayo yalibainishwa na mratibu wa Chanjo ya Shingo ya Kizazi Mkoani hapa Amos Kiteleja jana wakati akitoa semina kwa waandishi wa habari juu ya uanzishwaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi.

Alisema chanjo hiyo mpya haina madhara yoyote kwa watumiaji ambao ni mabinti wa kike kati ya umri wa miaka 9-14 na wanatajia kuwafikia zaidi ya mabinti zaidi ya 31000 walioko shuleni na nje ya shule mkoani hapa.

“Wazazi wasiwe na wasiwasi kwani chanjo hii ni muhimu sana kwa mabinti wa kike na inatolewa bure kuanzia Aprili 23 mwaka huu, kwenye hospitali ya wilaya Nyamagana (Butimba),’’ alisema.

Aidha alivitaja visababishi vya virusi hivyo kuwa ni kuanza kujamiana katika umri mdogo, mimba za utotoni, kuwa na wapenzi wengi, kuwa na ndoa za mitala, kuzaa watoto wengi na uvutaji.
Mratibu huyo pia alisema chanjo hiyo utatolewa mara mbili ili kupata kinga kamili na ya pili itatolewa mara baada ya miezi sita na itatolewa kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma ya afya, zahanati na sehemu zinapotolewa huduma tembezi na huduma ya mkoba hususani mashuleni.

“Saratani ya shingo ya kizazi huathiri via vya uzazi kwa wanawake na chanjo hii ya HPV huwakinga wasipate saratani hiyo pindi wawapo watu wazima na wakiwa na familia zao,’’ alisema.

Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk. Silasi Wambura alisema anategemea zoezi hili litafanyika kwa ufanisi wa hali ya juu ikiwa na kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

SHARE THIS

Facebook Comment