Monday, March 11, 2013

NESTA SANGA: MWIMBAJI NGULI KUTOKA DAR ES SALAAM NDANI YA TAMASHA LA PASAKA GOSPEL FESTIVAL 2013 CCM KIRUMBA TR 31/3/2013 NA TR 1/4/2013 CCM KATORO GEITA. JIONEE MWENYEWE ILI MACHO YAKO YAFAIDI KUELEKEA PASAKA MWAKA HUU MWANZA NA GEITA.NESTA SANGA.
Mwimbaji anayetisha katika medani ya muziki wa injili Tanzania kutoka Dar es Salaam Nesta Sanga amekuwa mwimbaji mwingine kuthibitisha kuimba katika Tamasha la Pasaka Gospel Festival 2013 litakalofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 31/3/2013 na tarehe 1/4/2013 katika uwanja wa CCM Katoro Geita.

Nesta ambaye kwa sasa anatamba na albamu yake mpya iitwayo TWENDENI ameweka wazi alipoongea na waandishi wa habari kuhusu maandalizi yake kuelekea tamasha hilo na kusema kuwa ashukuriwe Mungu ambae amempa nafasi katika tamasha hili la Pasaka Gospel Festival 2013.

Amesema kuwa yeye kama Nesta amejiandaa vya kutosha kuja kuwapa wakaazi wa Mkoa wa Mwanza na Mkoa wa Geita vitu vya ukweli ambavyo hawatakaa wasahau kamwe.

Pia amewaomba watu wote wa dini zote na wasiokuwa na dini kujitokeza kuja kujipa raha kaitka kusherehekea pasaka mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba na CCM Katoro Geita.

'' Nawaomba watu kuja siku hiyo kuona vipawa na nyimbo ambazo Mungu ametupa ili tuweze kubarikiwa kwa pamoja, na vilevile kumshukuru Mungu kwa ajili ya kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Yesu Mwokozi'' alisema Nesta.

Tamasha la Pasaka Gopsel Festival 2013 litawakutanisha waimbaji kutoka Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Arusha, Tabora, Mwanza na Geita. Waimbaji kutoka Dar es Salaam ni Enock Jonas[ Zunguka Zunguka] Neema Mwaipopo[ Raha Jipe Mwenyewe] Nesta Sanga[ Jiandaeni] Isaya Msangi[ Shetani Imekula kwako] Daniel Safari, John Shaban, Jessica Julius, Tumaini Mbembela kutoka Mbeya, Dan Sanga kutoka Iringa, Vedasto kutoka Tabora, Neema Munis kutoka Arusha na kwaya na bendi mbalimbali kutoka Mwanza na Geita.

Tamasha hilo litakuwa kwa gharama ya shilingi 2000/= kwa kila mtu katika maeneo yote ya Mwanza na Geita.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: