Saturday, November 10, 2012

Halmashauri ya wilaya ya Geita yagawanywa katika Halmashauri mbili.
Na Meshaki Mpanda-Geita


Waalimu 166 waliohamishiwa Halmashauri ya mji mdogo  elimu yao ni darasa la saba.


Baraza la Madiwani katika halmashauri ya Wilaya ya Geita  limegawanya halmashauri hiyo, kuwa halmashauri mbili  ambazo ni Halmashauri ya wilaya ya Geita na mji mdogo wa Geita.

Maamuzi hayo yamefanywa katika kikao cha Madiwani kilichofanyika Novemba7,mwaka huu,ambapo   mali na raslimali watu  viligawanywa kwa amani na utulivu kitendo  ambacho Mkuu wa mkoa wa Geita alikisifu na kukiri kwamba madiwani wameonyesha ukomavu.

 Katika mgawanyo huo,Halmashauri ya mji mdogo imepewa magari manne kati ya ishirini na saba yanayotembea na magari manne mabovu kama vitendea kazi.

Halmashauri  mpya ya wilaya yaNyang'hwale imepewa magari matatu yanayotembea ili yaweze kuisaidia wilaya hiyo  iliyoanzishwa mwanzoni mwa mwaka huu.

Katika kurahisisha usafiri  pikipiki 78 zliizokuwa zikitumiwa na watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo, kikao cha madiwani kilielezwa kuwa zitandelea kutumiwa na wafanyakazi wa halmashauri hizo mbili zilizogawanywa
Aidha   katika kuiongezea nguvu  halmashauri ya mji mdogo wa Geita  ilipewa pikipiki 15 ambazo zitatumika katika shughuli za ofisi.

Katika mgawanyo wa nyumba za watumishi,  halmashauri ya mji mdogo wa Geita  imepewa nyumba nne  ambazo zitatumiwa na wakuu wa idara, nyumba 21  zimegawiwa kwa wafanyakazi wa halmashauri ya  mji mdogo.

Kikao hicho kilichotawaliwa na amani kwa kiasi kikubwa kilipendekeza majengo yafutayo yapewe halmashauri ya mji mdogo ambayo ni, Ofisi za Maendeleo ya Jamii na Ushirika, jengo la mikutano GEDECO,kituo kipya cha mabasi, jengo linalotumiwa na AMREF,soko kuu,,machinjio ya Ihayabuyaga , mitambo ya maji Nyamalembo na kiwanja cha michezo cha Nyamiyengo.

Aidha kikao cha madiwani kilikubaliana madeni  ya watumishi wanayoidai halmashauri ya wilaya ya Geita ni shilingi milioni 455,560,324  yasilipwe mpaka kamati maalumu itakapoyahakiki na kuyathibitisha kuwa ni halali, kwa upande mwingine wazabuni nao wanaidai halmashauri ya Geita  shilingi bilioni 1,348,389,992 na yote hayajalipwa.

Katika mgawanyo wa madeni yote  kikao kilikubaliana kuwa robo tatu ya madeni yalipwe na halmashauri ya wilaya ya Geita na robo ya madeni hayo yalipwe na halmashauri ya  mji mdogo wa Geita.

 Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa katika taarifa ya Baraza hilo, waalimu 1,016 wa shule za msingi waliohamishiwa halmashauri ya mji mdogo, walimu 166 sawa na aslimia 16 wana kiwango cha elimu ya darasa la saba.
SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: